Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ANNE KILANGO MALECELA
amewaagiza wakuu wa shule za sekondari nchini kushirikiana na walimu
wapya wanaopangiwa katika shule zao ili waalimu hao wasiondoke katika
vituo vyao vya kazi.
Naibu Waziri huyo wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ametoa kauli hiyo
mkoani PWANI wakati akifungua mafunzo ya siku Tatu kwa wakuu wa shule
za sekondari nchini za serikali na zisizo za serikali mafunzo ya
kuwajengea uwezo wa juu uongozi na ufanisi katika shule wanaozoziongoza.
Naibu waziri huyo amewataka wakuu hao waangalie namna wanavyoweza
kufanya kazi na waalimu wapya wanaotoka vyuoni ili kuwafanya walimu hao
wapende kazi yao na wasitoroke katika vituo vyao vya kazi kwa visingizio
vya ugumnu wa mazingira.
Mapema akimkaribisha naibu waziri huyo, mtendaji mkuu wa wakala wa
maendeleo ya uongozi wa elimu nchini Dokta SISON MASANJA amesema
mafunzo hayo kwa wakuu wa shule za sekondari zote nchini yanalenga
kuwajengea uwezo juu ya uongozi na usimamizi fanisi wa shule zao.
Kwa upande wao wakuu hao wamekiri kupata changamoto kubwa pindi
wanapopokea waalimu wapya jambo ambalo wakati mwingine wanalazimika
kuwachukulia hatua za kuwawajibisha bila hata kuwashauri.
Home
News
Anne Kilango awaagiza Wakuu washule za sekondari kushirikiana na walimu wapya katika wanaopangiwa katika vituo vyao vya kazi
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment