Katibu wa Chama cha Watu wenye ulemavu wa Ngozi – ALBINO mkoani MBEYA -
WILLIAM SIMWALI amesema kuwa vitendo vya upigaji RAMLI mkoani humo
vitamalizika endapo serikali itawanyang’anya leseni waganga wa tiba
asilia wasio waadilifu.
SIMWALI ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya serikali
mkoani MBEYA kwa kushirikiana na wananchi kuanza zoezi la kuwabaini watu
wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya upigaji RAMLI mkoani humo.
Kwa mujibu wa takwimu za waganga wa tiba za asili mkoani Mbeya
wanafikia waganga zaidi ya 3,000 mkoa mzima, ambao wengine wanadaiwa
kwenda kinyume na kanuni na sheria za kazi zao.
Ofisi ya Mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya ndiyo inayohusika na kutoa
vibali vya waganga wa Tiba ya asili kupitia sheria Namba 23 ya mwaka
2002 ya Tiba ya asili nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment