Waziri Mkuu MIZENGO PINDA ameunga mkono juhudi za wananchi zaidi ya
1,600 wa Kijiji cha KIMONDO katika wilaya ya MBEYA ambao wameamua
kujenga Jengo la Zahanati kwa nguvu zao wenyewe, baada ya kutembea
umbali mrefu wa kufuata huduma za afya.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho cha KIMONDO baada ya kuweka
Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Zahanati hiyo, waziri Mkuu PINDA amesema
Serikali itaendelea kuboresha mazingira yay sekta ya afya hasa maeneo ya
Vijijini kwa lengo la kupunguza adha ya matibabu kwa wananchi.
Ujenzi wa Jengo hilo la zahanati ya kijiji cha Kimondo umeanza mwaka
2008 kwa kujitolea michango, mpaka sasa wananchi wamechangia shilingi
zaidi ya Milioni 34,Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imechangia shilingi
zaidi ya Milioni 7.
Waziri PINDA anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya, atakuwa wilayani
Kyela ambako pamoja na kuzindua miradi ya kuboresha zao LA mpunga wa
kyela, anatarajiai kukagua ujenzi wa chelezo katika bandari ya Itunge
mpaka wa Tanzania na Malawi.
Home
News
Waziri mkuu Pinda aunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na wananchi wa kijiji cha Kmondo Mbeya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment