Jeshi la polisi mkoa wa TANGA limetoa wito kwa wanahabari kuacha kutoa
taarifa zisizo sahihi kuhusu swala la majambazi waliokua wamejificha
kwenye pango lililo jirani na mapango ya utalii ya amboni,wiki moja
iliopita.
Kamanda wa Polisi mkoa wa TANGA, FRAISHER KASHAI ametoa wito huo
katika kikao chake na waandishi wa habari. Mwandishi wetu BERTHA
MWAMBELA alihudhuria mkutano huo na hii ni taarifa yake.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa
Tanga Fraisher Kashai amesema wapo baadhi ya wanahabari wanatoa taarifa
zisizo sahihi jambo linalosababisha hofu kwa wakazi wa Tanga,na hata
wageni wanaokuja kufanya shughuli za utalii katika mapango ya amboni.
Jambo jingine lililozungumzwa na kamanda Kashai ni namna
walivyojipanga kudhibiti hali ya wageni wanaoingia kwenye makazi ya watu
bila taarifa kuanzia ngazi ya kata.
Hata hivyo jeshi la polisi linawashikilia watu kadhaa kutokana na
uporaji wa silaha kwa askari polisi wawili waliokua doria tarehe 26
mwezi wa kwanza mwaka huu.
Home
News
Waandishi wahabari watakiwa kutumia kalamu zao kuandika habari za kweli kuliko kupotosha Umma
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment