Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu, tawala za mikoa na serikali za mitaa ( TAMISEMI ) Jumanne Sagini amesema hatasita kuchukua hatua stahiki, ikiwemo kuwafukuza kazi baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, manispaa na majiji watakaobainika kushindwa kusimamia matumizi ya fedha za umma na miradi inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo.
Ametoa onyo hilo wakati akifunga mafunzo ya sheria mpya ya ununuzi wa umma yaliyowashirikisha wajumbe wa bodi za ununuzi, wanasheria na wakurugenzi wa halmashauri nane zinazotekeleza mradi wa uimarishaji wa miji 18 ya tanzania bara, yaliyofadhiliwa na benki ya Dunia kwa ushirikiano na taasisi ya kiufundi ya ubelgiji kwa lengo la kuzijengea uwezo halmashauri hizo katika kuandaa na kusimamia mifumo ya ununuzi kwa weledi na tija zaidi.
>>>>Bofya hapa kujua zaidi http://www.itv.co.tz/news
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment