Image
Image

Achana na mimi ya tunda man yaziweka kiporo kamanda ya Daz Nundaz na Mkasa wa Bosi


Mwana muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Tunda amefunguka juu ya dhamira yake  na dhumuni la kurudia nyimbo mbili anazozipenda sanaa zilizoibwa na Ferooz katika kipindi cha nyuma kidogo  ukiwemo wimbo wa ‘Kamanda’ wa Daz Nundaz pamoja na Mkasa wa Boss’ wa kwake Ferooz.
Moja ya sababu ambayo imemfanya kuzirudia kuimba nyimbo hizo tundamani licha ya sababu ya mwanzo aliyosema kuwa nikuzipenda amesema kuwa pia anataka ziwe na mahadhi ya kisasa zaidi kusudi ziweze kuwa na ubora wa namna flani kwani huku akitolea mfano wimbo wa kamanda ambao amesema kuwa wimbo huo ulikuwa unapigwa katika stesheni ama vituo mbali mbali vya radio kwa wakati wote lakini kwa sasaivi inakuwa ni nadra kupigwa ila unakuwa unapigwa wakati maalumu pengine umetokea msiba lazima uusikie na nyimbo nyingine za aina hiyo.
Kupitia kipindi cha Leo Tena Clouds Fm amefunguka hayo wakati alipokuwa  akitambulisha ngoma yake mpyaaa kutoka kwenye maganda yake inayokwenda kwa jina la ACHANA NA MIMI.
Tunda alisema kuwa nyimbo hizo atazibadilisha lakini anatuliza akili kwa kutafuta maneno yakuweka kwenye nyimbo hizo ila melody atatumia hiyo hiyo huku akisema katika nyimbo ambazo alikuwa anataka kuanza nazo ila zikawa zinampa  ugumu kidogo  wa kutafuta kisa cha kukiweka ni Mkasa wa Boss na Kamanda  ambao anaona kama zimesheheni kila kitu  ndani yake.
Amesema kuwa atahakikisha kuwa kwa taratibu tu akiwa anachekecha bongo yake kutafuta maneno ama kisa chakuimba  kwenye nyimbo hizo anataka aziimbe vizuri ili ziweze kuwakonga nyoyo za  mashabiki wake bila kupoteza ladha halisi za nyimbo hizo.
Aidha katka hatua nyingine tunda mani wakati akiulizwa juu ya namna anavyo badilika badilika katika muziki kwa sasa tofauti na kipindi cha nyuma ambapo nyimbo nyingi alikuwa anaimba za kulalamika amesema kuwa  anabadilika ili kuwapa ladha mashabiki wake wote bila kuwabagua nakusema kuwa”Ujue nyimbo zangu za kulalamika hizi mara nyingi ninapo enda katika shoo lazima niimbe watu nao wanazipenda kwakuwa nawakumbusha kipindi cha nyuma”Alisema Tunda mani.
Tunda mani amekuwa akiimba Qaswida ama nyimbo za dini ya kiislam anaulizwa kwakuwa na hizi unapenda kuziimba na unauwezo nazo vipi unampango wa kuziacha nyimbo za kidunia ukaingia huku ama ipoje hii”Hapana sina mpango wa kuacha nyimbo za kidunia ila tambua kwamba hizi nyimbo naimba na tayari naandaa albam ya nyimbo za dini yaani Qaswida kimfano kipindi cha ramadhani na kipindi kingine zinatumika,ila itafikia wakati nitatoka kwenye nyimbo za kidunia na kuingia hizi za kumuabudu mwenyezi mungu kwa hiyo nipo mguu ndani mguu njee”Alisema Tunda Mani.
Amewaomba pia mashabiki kuupokea ujio wake huo mpya wa achana na mimi ambao anaamini utafanya vizuri zaidi kwa kuwa ushaanza kuonyesha matumaini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment