Waziri Mkuu MIZENGO PINDA ametembelea baadhi ya familia zilizopoteza
wapendwa wao pamoja na majeruhi waliolazwa kwenye hospitali ya wilaya ya
KAHAMA kutokana na maafa ya mvua ya mawe iliyonyesha usiku wa
kuamkia jana.
Akizungumza na wafiwa katika vijiji vya MWAKATA na MAGUGUNG’HWA
wilayani KAHAMA Waziri Mkuu amesema serikali haitawaacha katika kipindi
hiki kigumu na kwamba serikali imepanga kupeleka vyakula, mahema,
mablanketi na dawa ili kuwasaidia waathirika hao.
Waziri Mkuu PINDA ameagiza maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula - NFRA yaliyoko ISAKA kupokea misaada
ya chakula ili kuratibu misaada kwenda MWAKATA ambapo maafa yametokea.
Aidha taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
imesema serikali inapokea misaada mbalimbali kwa ajili waathirika na
misaada hiyo inaweza kuwasilishwa Idara ya Kuratibu Maafa, Ofisi ya
Waziri Mkuu DSM au kuwasilisha katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
SHINYANGA.
Zaidi ya watu 40 wamekufa na wengine zaidi ya 90 kujeruhiwa baada ya
mvua ya mawe kunyesha Jumanne usiku katika kata ya MWAKATA wilaya ya
KAHAMA mkoani SHINYANGA.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment