Serikali imesema inaendelea kutoa kipaumbele kwa Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa -BRN katika kutekeleza majukumu yake na kuhakikisha sekta
na miradi inayotambuliwa na kuingizwa ni ile yenye manufaa na ya haraka
kwa wananchi wengi.
Akizindua taarifa ya mwaka ya matokeo ya utekelezaji wa mpango huo
jijini DSM Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema mpango huo una uwezo wa
kufanikisha mambo mengi kwa muda mfupi na kufikia malengo yaliyowekwa
kwa haraka zaidi.
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ambao Serikali imezindua ripoti ya
kwanza ya utekelezaji wake jijini DSM iliyoainisha mafaniko
yaliyopatikana katika Sekta SITA za mwanzo za kipaumbele kwa mwaka
2013/2014.
Mbunifu wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa Mtendaji Mkuu Ofisi ya
Rais Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi -PDB OMAR ISSA amesema mfumo huo
ni wa wazi ambao umeleta nidhamu katika utendaji kazi na kueleza ripoti
hiyo kabla ya kuzinduliwa kampuni binafsi ilifanya uchunguzi na
kugundua vilivyoelezwa kwenye ripoti hiyo ni kweli.
Mashuhuda wa BRN nao wakatoa ushuhuda wao jinsi mpango huo
ulivyowasaidia hususan katika kupatiwa mafunzo yaliyoweza kubadilisha
masuala mbalimbali ikiwemo kilimo na ufundishaji.
Mikakati hiyo ya BRN ilitekelezwa kwa mujibu wa Mpango kazi wa miaka mitatu ambao ulizinduliwa mwaka 2013.
Home
News
Serikali imesema itaendelea kutoa kipaumbele kwa mpango wa BRN katika kutekeleza majukumu yake
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment