Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha miswada
miwili ya sheria ya usimamizi wa maafa ya mwaka 2014 pamoja na ule sheria
ya usimamizi wa kodi wa mwaka huo huo 2014.
Miswada hiyo imepitishwa baada ya kushindikanika katika vikao
vilivyopita kutoka na idadi ya wabunge waliotakiwa kuipigia kura kutokutimia.
Mapema leo ,Mwenyekiti wa bunge Lediana Mng'ongo ametoa agizo kwa
wabunge waliopo nje ya bunge kuingia ndani ili idadi inayotakiwa kisheria
kupigia kura muswada wa marekebisho ya sheria ya uhamiaji ya mwaka 2014 ambao
inahitaji robo tatu ya wabunge wawepo wakati unapitishwa.
Kumekuwa na mahudhurio yasiyoridhisha ya wabunge katika mkutano wa
19 ambao unaendelea mkoani Dodoma hali inayofanya baadhi ya miswada
kushindikanika kupitishwa.
0 comments:
Post a Comment