Ubalozi
wa Marekani nchini Uganda umetoa tahadhari ya dharura kwa raia wake nchini
Uganda hapo jana inayosema kuwa kunauwezekano wa kuwepo kwa tishio la kigaidi
Jijini Kampala.
Ubalozi
wa Marekani umepata taarifa za kuwepo kwa uwezekano wa tukio la shambulizi la
kigaidi eneo ambalo raia wa nchi za magharibi wakiwemo wa Marekani hupenda
kukaa Jijini Kampala, na tukio hilo linaweza kufanyika mapema mno.
Ubalozi
wa Marekani haujatoa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo, lakini nchi ya
Uganda ambayo ni rafiki na Marekani na yenye majeshi yake nchini Somalia
ilishashambuliwa siku za nyuma na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab.
0 comments:
Post a Comment