Polisi wa Ufaransa wamesema hali mbaya ya hewa ya milima ya Alps
ilipoanguka ndege hiyo , huenda
ikasababisha ichukue siku kadha kuipata miili hiyo.
Wachunguzi wanasema mahali ilipoanguka ndege hiyo panaogopesha mno
na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani , amezungumzia picha za kutisha za ajali hiyo.
Ndege hiyo aina ya Airbus A
320 ilitokea Barcelona, Hispan ia ikiwa ina kwenda Duesseldorf, Ujerumani , na
miongoni mwa abiria walikuwemo Wajerumani 60 na raia 45 wa Hispania ambayo
imetangaza siku tatu za maombolezo.
Wakati huo huo , Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Ufaransa imetangaza kupatikana kwa kisanduku cha ndege hiyo
chenye vifaa vinavyorekodi mawasiliano na matukio ya ndege inapokuwa angani .
0 comments:
Post a Comment