Shambulio hilo jipya limetokea kwa mtoto wa kiume Baraka Cosmas wakati alipokuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda amesema kwa sasa mtoto huyo anapata matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri.
Polisi inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika.
Shambulio hilo linajitokeza wiki moja tu baada ya watuhumiwa wanne kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa mauaji ya albino, Na muda mfupi baada ya Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kupitia hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa pili mwaka huu kukemea mauaji ya albino, ambao viungo vyao hutumika katika shughuli za kishirikina kwa imani potofu kuwa zinasaidia kuleta utajiri na madaraka.
0 comments:
Post a Comment