Mali imeapa kutosalimu amri kwa ugaidi na kwamba itawaadhibu wapiganaji wa jihad
Mali imeapa kutosalimu amri kwa ugaidi na kwamba itawaadhibu wapiganaji wa jihad waliohusika na shambulio la maafa kwenye klabu moja ya usiku katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bamako ambapo watu watano waliuawa.
Mali imekuwa katika tahadhari ya hali ya juu tangu mtu aliyekuwa na silaha
nzito kuingia kwenye klabu hiyo ya usiku mahali wanapotembelea sana wageni
na kuua watu watano akiwemo raia mmoja wa Ufaransa na mwingine kutoka
Ubelgiji.
Kikundi cha kupambana na ugaidi kutoka Ufaransa kimewasili Mali kuungana na
majeshi ya nchi hiyo katika uchunguzi na kumsaka muuaji huyo na mtuhumiwa
mwingine aliyekuwa naye.
Msemaji wa serikali ameapa kuwa kamwe Mali haitavumilia vitendo vya kigaidi
na kuomba waasi wa kabila la Tuareg kwenye maeneo tete ya kaskazini mwa Mali
kutia saini mkataba wa amani uliotiwa saini na serikali tarehe mosi mwezi
huu.
0 comments:
Post a Comment