Wanajeshi wa Chad na Niger wamewaua wapiganaji 300 wa kikundi cha Boko Haram
na wao wamepoteza wanajeshi 15 wakati wa kuteka miji miwili iliyoko
kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Wapiganaji hao wamekuwa wakishikilia miji hiyo ya Malam Fatouri na Damasak
karibu na mpaka wa Niger tangu mwezi Novemba mwaka jana na katika mapigano
hayo wanajeshi 30 wa Niger na Chad pia walijeruhiwa.
Mapigano ya kuteka miji hiyo yamekuja siku moja baada ya maelfu ya wanajeshi
wa Chad na Niger kuvuka mpaka na kuingia maeneo ya kaskazini-mashariki mwa
Nigeria kuchukua maeneo yaliyokuwa yanashikiliwa na wapiganaji hao.
Mapigano hayo pia yamekuja wakati Umoja wa Afrika ukiridhia kuundwa kwa
kikosi cha kanda cha askari 10,000 kuungana katika mapambano na kikundi cha
Boko Haram ambacho mwishoni mwa wiki kiliahidi kuwa mtiifu wa kikundi cha Islamic State chenye wapiganaji wa jihadi huko Syria na Iraq.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment