Aliyekuwa Mke wa rais wa Ivory
Coast, Simone Gbagbo amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa
kuhusika na machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka
2010.
Simone Gbagbo, mwenye umri wa miaka
65, alifunguliwa mashtaka ya kudharau usalama wa taifa.
Mumewe aliyekuwa rais wa Ivory
Coast, Laurent Gbagbo, naye anangojea kushtakiwa katika Mahakama ya
Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Zaidi ya watu 3,000 walikufa kwenye
machafuko yaliyofuatia baada ya uchaguzi wa rais, kufuatia Gbagbo
kupinga kushindwa na Alassane Ouattara.
0 comments:
Post a Comment