Mkuu wa mkoa wa ARUSHA, FELIX NTIBENDA ameridhishwa na hatua ya
maandalizi ya ujenzi wa jengo la kuhifadhia nyaraka na kumbukumbu za
mwenendo wa kesi za makama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari.
NTIBENDA akizungumza mara baada yakutembelea eneo la LAKIL LAKI
ambako ndiko ujenzi huo utafanyika,amesema tayari mkandarasi wa ujenzi
huo ameshafika katika eneo hilo na vifaa vya kwa ajili ya kuanza ujenzi
huo vimeshawasili na ujenzi unatarajia kukamilika katika kipindi cha
mwaka MMOJA.
Mkuu huyo wa mkoa wa ARUSHA, FELIX NTIBENDA amesema mradi huo
unatarajia kukamilika mwezi machi mwakani na utaanza katika kipindi cha
siku KUMI na TANO.
Mkandarasi wa ujenzi huo,amesema wanatarajia kujenga majengo hayo ambayo yatakuwa mfano kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya ARUSHA, FIDELIC LUMATO amesema iwapo
ujenzi huo ukimalika utachangia kwa kiasi kikubwa kuleta maenedeleo kwa
wananchi wanaoishi katika eneo hilo.
Ekari 436 zimetengwa na halmashauri ya ARUSHA kwa ajili ya ofisi mbali mbali za kimataifa .
Home
News
Mkuu wa mkoa wa ARUSHA FELIX NTIBENDA aridhishwa na ujenzi wa jengo la kuhifadhi kumbukumbu ya mauaji ya kimbari.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment