Serikali ya CHINA imesema itaongeza nguvu katika uhusiano wake na
mataifa ya AFRIKA katika sekta kuu muhimu ikiwemo viwanda, afya na
kuimarisha usalama na amani ambapo TANZANIA ni miongoni mwa nchi za
AFRIKA ambazo tayari zimetiliana saini mikataba mbalimbali ya maendeleo
na nchi hiyo.
Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa CHINA, WANG YI katika
mkutano na waandishi wa habari ukiwa ni mwendelezo wa mawaziri wa CHINA
kujibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu utendaji wa kazi za wizara
zao katika kipindi hiki ambacho bunge la watu wa CHINA (NPC)
likiendelea na vikao vyake.
waziri WANG LI anasema CHINA itaendelea na ushirikiano hususani
kuyapa nguvu maendeleo ya viwanda, kuimarisha ushirikiano katika sekta
ya afya kwa kujenga uwezo kwa waafrika kuweza kupambana na magonjwa
mbalimbali yamlipuko ikiwa ni panoja na kusaidia bara la AFRIKA
kudumisha amani na usalama kwa kujua nyenzo muhimu za kupamba na
kukomesha makundi mbalimbali yakiwemo ya kigaidi na vita vya wenyewe
kwa wenyewe.
March 2013 wakati wa ziara ya rais wa CHINA XI JINPING nchini
TANZANIA, serikali ya CHINA na TANZANIA zitiliana saini ya ushirikiano
katika masuala mbalimbali yakiwemo kilimo, mawasiliano, nishati na
miundombinu.
Aidha waziri WANGI LI amesema CHINA itaendelea na mchango wake kutoa
misaada ya hali na mali katika kupambana na ugonjwa wa EBOLA
unayoyakabili mataifa ya AFRIKA MAGHARIBI.
Tayari nchi ya CHINA imepeleka wataalamu 100 wa afya katika mataifa
yaliyoathiriwa na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa dola
za MAREKANI milioni 122 kwa mataifa hayo.
Mwezi uliopita CHINA iliteua mwakilishi wa kudumu katika umoja wa
AFRIKA (AU) ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kuimarisha mahusiano na
bara la AFRIKA.
Mawaziri mbalimbali kutoka bara la AFRIKA na wale wa CHINA
wanatarajia kukutana katika Mkutano wa sita kuhusu ushirikiano wa
AFRIKA na CHINA (FOCAC) unatarajia kufanyika baadae mwaka huu nchini
AFRIKA KUSINI.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment