Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge
wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais amefanya uteuzi
huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya
66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.
Walioteuliwa ni
Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba, Uteuzi huu umekamilisha idadi
ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa
kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.
Wabunge
ambao wameshateuliwa ni:
-
Mhe.
Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
-
Mhe.
Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
-
Mhe.
Dkt. Asha Rose Migiro
-
Mhe.
Janet Zebedayo Mbene
-
Mhe.
Saada Salum Mkuya
-
Mhe.
Zakhia Hamdani Meghji
-
Mhe.
Shamsi Vuai Nahodha
-
Mhe.
James Fransis Mbatia
Uteuzi huu
umeanza tarehe 20 Machi, 2015.
……………………………MWISHO……………………………….
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa
Rais, Msaidizi
Ikulu-Dar-Es-Salaam
26 Machi, 2015
0 comments:
Post a Comment