Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
jioni ya Jumatano, Machi 18, 2015 amewasili nchini Burundi kwa ziara ya
kikazi ya siku mbili nchini humo.
Kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mji mkuu wa Burundi wa Bujumbura, Rais
Kikwete amepokelewa na Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza na
pamoja na mamia kwa mamia ya wananchi wa Burundi.
Rais
Kikwete ambaye amewasili Burundi akitokea Dodoma ambako alikuwa katika
ziara ya kikazi pia leo Machi 19, 2015, atahutubia Bunge la Nchi
Wanachama wa Afrika Mashariki (EALA) katika nafasi yake ya Uenyekiti wa
Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC)
katika hotuba ya The State of the East African Community Address.
Saa
chache baada ya kuwasili Bujumbura, Rais Kikwete amehudhuria chakula
cha jioni ambacho ameandaliwa na Rais Nkurunzinza kwenye Hoteli ya
Panoramique.
Wabunge wa Bunge la EALA pia wamehudhuria chakula hicho cha jioni.
Home
News
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment