Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi
kufungua rasmi Kituo cha Taifa Cha Kumbukumbu kilichopo Kisasa mjini
Dodoma leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia jalada la mwaka 1940 ambapo
alisoma utendaji kazi wa Babu yake Chifu wa Kabila la Wakwere Mrisho
Kikwete wakati huo.Jalada hilo ni moja ya majalada ya zamani
yaliyohifadhiwa kutumia teknolojia ya kisasa katika Kituo Cha Taifa Cha
Kumbukumbu kilichopo Kisasa mjini Dodoma.Katika hotuba yake wakati wa
ufunguzi wa kituo hicho Rais Kikwete ametoa agizo la kuanzishwa maktaba
za Viongozi wa kitaifa hususan marais wastaafu ili kuhifadhi vyema
historia ya nchi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa
Kituo cha Taifa Kumbukumbu huko kisasa mjini Dodoma leo.Wapili kushoto
ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, watatu kushoto ni
Mwenyekiti wa BungeMh. Zungu na kulia ni Waziri wan chi Ofisi ya Rais
Utawala BoraMh.George Mkuchika.
(Picha na Freddy Maro)
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment