Naibu
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi,PEREIRA AMME
SILIMA ameliambia Bunge
kuwa Tanzania haina mkataba na China wa kubadilishana wafungwa.
Amesema
ni nchi mbili tu ambazo zilikuwa na mkataba na Tanzania , wa kubadilishana wafungwa , ambazo Thailand na Mauritius , ambazo hata hivyo mikataba hiyo imekwisha.
Naibu
Waziri huyo wa Mambo ya
Ndani ya Nchi alikuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum , REBECCA MNGODO aliyetaka kujua idadi ya Watanzania
wanaotumikia vifungo nchini China
]na uwezekano wa kurejeshwa kutumikia vifungo vyao hapa nyumbani.
Wakati huo huo, Serikali imewasilisha bungeni muswada wa sheria ya
kudhibiti silaha wa mwaka 2014 ambapo kupitia muswada huo kutakuwa na ukomo wa
kumiliki silaha pamoja na kutambuliwa silaha zinazotengenezwa kienyeji.
Akiwasilisha muswada huo Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Pereira Silima amesema kumekuwa na mapungufu makubwa katika umilikaji wa silaha hivyo kupitia muswada huo anatumai silaha zitamilikiwa katika utaratibu muafaka zaidi.
Kwa upande wake kaimu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya ulinzi na usalama Kapteni Mstaafu John Chiligati amesema moja kati ya mambo ambayo yatasaidia udhibiti wa umilikaji holela wa silaha ni wamiliki wote kutambulika bila kujali kama ni silaha zilizotengenezwa kienyeji au la.

Naye
msemaji kambi ya upinzani katika kamati hiyo godbless lema amesema muswada huo
siyo suluhu ya udhibiti matumizi holela ya silaha bali Serikali inatakiwa
kutenda haki kwa wananchi wote kwani baadhi yao huzitumia silaha hizo katika
kudai kile wanachodhani ni haki kwao.
0 comments:
Post a Comment