Image
Image

Tamwa kukutana na wahariri kujadili ukatili unaosababishwa na ulevi wa pombe kupindukia

Na Mwandishi wetu.
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA leo tarehe 20 Machi, 2015 saa 3:00 asubuhi kinakutana na Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali kujadili mikakati kwa kutumia vyombo vya habari ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyosababishwa na unywaji pombe kupindukia. 
Mkutano huo wa TAMWA na Wahariri utajadili njia zitakazotumika kwa jamii ili kuweka uelewa wa madhara ya unywaji pombe kupindukia kwani unachangia ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto na kurudisha maendeleo nyuma.
 Akizungumza; Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi – CRC kilichoko ndani ya TAMWA Bi. Gladness Munuo amesema kwa mwaka mzima wa 2014,  kilipokea kesi 107 za vitendo vya ukatili wa kijinsia vilivyosababishwa na ulevi wa pombe kupindukia ambapo kati ya hizo wanawake walikuwa 80, wanaume 22 na watoto walikuwa ni watano. 
Aidha katika mkutano huo; Wahariri watajadili mbinu jinsi ya kukuza uelewa wa jamii juu ya madhara ya unywaji pombe kutokana na kuwa baadhi ya wanaume wamekuwa wakitelekeza familia zao na kuacha wanawake wakihangaika na watoto.
Akizungumza na  mwandishi wetu, Bi. Munuo alisema vyombo vya Habari vikitumika katika kutoa elimu ya madhara ya unywaji pombe hasa kwa ukatili ambao umekuwa ukifanywa kimya kimya vinaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ndani ya jamii
Bi Munuo aliutaja ukatili unaofanywa kimya kimya kuwa ni wa kingono, ubakaji na vipigo ambao unafanyika ndani ya familia huku idadi ya wanawake na watoto kutelekezwa ikiendelea kuongezeka.
Aidha baadhi ya wanandoa wamekuwa wakitumia kilevi kupindukia na kusababisha wengine kushindwa kuwahudumia watoto wao ki - afya, kukosa chakula na mahitaji mengine kama ada za shule hali ambayo husababisha taifa kupoteza nguvu kazi.
Mkutano huo ni mwendelezo wa mikakati ya kupinga vitendo vya ukatili unaosababishwa na  nywaji pombe kupindukia katika kukuza uelewa wa jamii ili kuwezesha kutoa taarifa za matukio hayo pamoja na madhara ya kiafya na maendeleo kupitia Habari, vipindi vya redio na televisheni.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment