Habari kutoka nchini ZAMBIA, zinasema rais wan chi hiyo EDGAR LUNGU
amefanyiwa upasuaji wa koo akiwa nje ya nchi alikolazimika kupelekwa
baada ya kuugua ghafla.
Awali madaktari wanaotibu nchini humo walidau kuwa LUNGU alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
Kiongozi huyo wa ZAMBIA aliyechaguliwa mwezi januari kuliongoza
taifa hilo, alianguka na kuzimia jana jumapili, alipokuwa akitoa hotuba
mjini LUSAKA, wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
LUNGU alikimbizwa hospitalini baada ya tukio, na madaktari
wakaidhinisha kuwa apatiwe matibabu ya haraka nje ya nchi. Wakati wa
kampeni za uchaguzi wapinzani walidai kuwa LUNGU mwenye umri wa miaka 58
ni mgonjwa, taarifa ambazo mwenyewe alizipinga.
Rais huyo wa ZAMBIA alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo baada ya kifo
cha aliyekuwa rais wan chi hiyo MICHAEL SATA, kutokana na maradhi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment