Dunia imelaumiwa kwa kushindwa
kuitikia haraka kutoa msaada wa kupambana na mlipuko wa ugomjwa wa EBOLA
uliotokea Afrika Magharibi na kuchangia kuenea haraka kwa ugonjwa huo na kuuawa
zaidi ya watu 10,000 kufikia mwezi huu.
Katika ripoti ya kuadhimisha
mwaka wa kwanza tangu kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa huo shirika la hisani la
madaktari wasiokuwa na mipaka limesema taasisi nyingi zilishindwa kuchukua mkakati
unaolenga athari ambazozingeepukwa.
Mwezi Januari mwaka huu kwenye
mkutano wa dharura usio wa kawaida Shirika la Afya Duniani lilikiri kuchelewa
kuitikia mlipuko huo na Mkurugenzi Mkuu wake DR. MARGARET CHAN anasema dunia
pamoja na lishirika lake walikuwa goi goikuona kilichokuwa kinatokea mbele yao.
Katika miezi 12 iliyopita ugonjwa
huo umeua watu 10,251 kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani
iliyotolewa tarehe 18 ya mwezi huu na wengi wao wakiwa Liberia zaidi ya 4000,
Sierra Leone zaidi ya 3,700; Guinea zaidi ya 2,000 na Nigeria watu wanane.
0 comments:
Post a Comment