Kiongozi wazamani wa Singapore, Lee Kuan
Yew, ambaye aliibadilisha nchi hiyo kutoka mji wa bandari na kuwa taifa lenye
uchumi mkubwa duniani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.
Waziri huyo mkuu wa taifa hilo kwa
miaka 31, alikuwa akiheshimiwa mno kama mratibu wa maendeleo ya Singapore.
Hata hivyo alikosolewa kwa kuongoza
kwa mkono wa chuma, ambapo wakati wa utawala wake uhuru wa kutoa maoni ulibanwa
huku wapinzani wa kisiasa walikuwa wakifikishwa mahakamani.
Maziko ya kitaifa ya Lee Kuan Yew,
yatafanyika machi 29, baada ya wiki moja ya kuomboleza.
0 comments:
Post a Comment