Rais wa Zanzibar na
mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr.Ali Mohmaed Shein amesema ahadi alizozitoa
za afya asilimia kubwa zimetekelezwa ikiwemo ya kitengo cha
matibabu ya ubongo na uti wa mgongo.
Dr. Shein ametoa kauli hiyo
ikulu wakati alipokutana na madakatari bingwa wa kichwa na uti wa
mgongo na Afrika mashariki ambao walifika ikulu kuonana naye,ambapo Dr Shein
amemsmea kati ya ahadi tatu aliozoziahidi wkati akifungua baraza la wawakilishi
mwaka 2010 mara baada ya kuunda serikali aliahidi kuanizsha huduma tatu
ambazo ni upasuaji wa Moyo,matibabu ya njia za chakula na maradhi ya njia
za mkojo na figo ambapo ni huduma ya upasiaji wa moyo pekee ndiyo
mandalizi hayajakamilika huku akifurahishwa na hatua za kitengo cha
kichwa na uti wamgongo kuwa ni moja ya kituo kikubwa afrika
mashariki.
Kwa upande wake Daktari
bingwa wa upasuaji mishipa Dr.Mahmuod Qureshi amesema taasisi hiyo ya Zanzibar
ni muhimu sana na ndio maana wataalamu wengi wamekuja kujifunza
hapo.
Kwa upande wake
mkurugenzi mkuu wa hospitali ya mnazi mmoja Dr. Jamala Adam Taibu amesema
tayari kituo hicho kimeshafanya upauaji wa wagonjwa 713 wakiwemo watoto 212
waliofanyiwa upauaji wa vichwa na 78 uapasuaji wa uti wa mgongo,huku
wengine 62-ubongo,uapsuaji wa uti 183 hukuwengine wakifanyiwa upauaji wa
kuondoa uvimbe wa mafuta na Saratani ya damu.
0 comments:
Post a Comment