Mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida,imewahukumu
madereva wanne wa magari ya abiria na mizigo, adhabu ya kutumikia jela
jumla ya miezi kumina mbili na kulipa faini ya jumla ya shilingi elfu
themanini baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka sheria za usalama
barabarani ikiwemo ya kuendesha magari yakiwa mabovu,kuegesha maeneo yasi
ruhusiwa na kujaza abira wengi kupita kiasi jambo ambalo
linahatarisha maisha ya abiria..
Mwendesha mashitaka na mwanasheria wa
serikali,Pridence Mutta,alidai mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo,Joyce
Minde kuwa mnamo aprili 20 mwaka huu majira ya asubuhi huko katika kata ya
Ipembe mjini hapa,dereva Willson John miaka ishirini na tatu mkazi wa
kititimo manispaa ya singida,alikamatwa akiwa amepakia abiria wengi kwenye lori
dogo aina ya fuso lenye usajili wa namba T.354 BGX kinyume na
Sheria.
Naye dereva wa FUSO T.674 ERM Simon
David miaka thelathini na Saba mkazi wa moshi mjini mkoani
kilimanjaro,amepatikana na hatia ya kuendesha gari na magurudumu yake yakiwa
yamechaa na kiti cha dereva kibovu hakifai,pia mshitakiwa wa mwisho Bwana Juma
Ramadhani miaka ishirini na mbili mkazi wa mtinko jimbo la Singida
kaskazini,amehukumiwa kwenda jela miezi mitatu baada ya kukutwa akiendesha gari
likiwa katika hali mbaya.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu,mwendesha mashitaka
Mutta aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washitakiwa itakayokuwa
fundisho kwake na madereva wengine ambao hawatii sheria za usalma barabarani na
kuhatarisha maisha ya wananchi.
Hakimu Minde,alisema ili kuondoa dhana iliyoota
mizizi kwa baadhi ya madereva kwamba makosa ya usalama barabarani, adhabu yake
ni kulipa faini tu na mshitakiwa anao uwezo wa kulipa na kuachiwa huru, kwa
hiyo washitakiwa wote wanne kila moja amepewa adhabu ya kwenda jela miezi
mitatu na akimaliza adhabu ,atalipa faini ya shilingi elfu ishirini
ndipo urudi nyumbani kwake.
Aidha hakimu Ninde amesema kwa sasa hali
ni mbaya kila siku ni ajali ambazo zinazopoteza nguvu kazi na
kuziacha familia bila kuwa na wategemezi,hii yote inasababishwa na madereva
kutokutii sheria za usalama barabarani na wakati mwingine mahakama nazo
kutokutimiza wajibu wake ipasavyo kwa kutoa adhabu ya faini badala ya
kifungo pamoja na faini.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani
mrakibu msaidizi wa polisi ASP JOSEPH BUKOMBE amesema wameamua
kuchukuwa jukumu la kuwapeleka mahakamani na bila ya kuwatoza faini kwa sababu
makosa yao yamekuwa yaki jirudia kila wanapo kamatwa.
Katika hatua nyingine ASP BUKOMBE amesema
wamekamata pikipiki na bajaji zaidi ya thelathini na tano zilizo
kuwa na makosa kwa lengo la kuwataka waajiri wa pikipiki hizo kufika kituoni
ili washitakiwe wao na madereva wao ambao wengi wao wamekuwa wakiendesha
bila leseni,kuvunja sheria za barabarani nakusababisha ajali ambazo zina
garimu maisha ya abiria bila sababu.
Kwaupande wao baadhi ya madereva walio fika
mahakamani kwa ajili ya kujaribu kuwawekea dhamana wenzao na zoezi hilo
kugonga mwamba wamesema kuwa barabara zote katikati ya manispaa ya Singida
hakuna sehemu ambayo kuna kibao cha kuegesha gari , kwahiyo wameiomba
manispaa ya Singida kuweka vibao na kutenga maeneo ya maegesho,kwani
kwasasa wamekuwa wakikamatwa wanapo egesha magari na askari wa usalama
Barabarani.
0 comments:
Post a Comment