Dokta slaa ameyasema
hayo mjini Morogoro wakati akihutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya
Morogoro katika uwanja wa kiwanja cha Ndege ambapo amesema kudumisha
muungano si kusherekea bali ni kufanya mambo ambayo yataweza kudumisha muungano
huo na kusema kuwa lazima muungano uwe wa serikali tatu ambapo
amewataka wananchi wa mkoa wa morogoro kuunga mkono jitihada za ukawa kwa
kupiga kura ya hapana katiba inayopendekezwa.
Kuhusu maadhimisho ya
siku ya wafanyakazi yaani Mei Mosi yatakayofanyika kitaifa jijini Mwanza ambapo Dr
Slaa amesema amealikwa lakini haoni sababu ya kushiki kutokana na
serikali kupuuza madai ya msingi na haki za
wafanyakazi kwa muda mrefu ambapo amewataka wafanyakazi
kufanya maamuzi magumu kuipa nafasi serikali itakayosimamia
malalamiko ya wafanyakazi kwa vitendo.
0 comments:
Post a Comment