Image
Image

Serikali yawatangazia kiama wazazi ambao wamewazuia watoto wao kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu .



Serikali wilayani butiama imetangaza kuchukua hatua kali za kuwakamta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wazazi ambao wamewazuia  watoto wao kujiunga  na  kidato cha kwanza mwaka huu  kisha kuwaonza huku jeshi la polisi,viongozi wa vijiji na kata  wakiagizwa  ifikapo mwisho wa  mwezi huu kuanza msako wa nyumba hadi nyumba.
Agizo hilo la serikali limetolewa na mkuu wa  wilaya ya butiama mkoani mara Bi Annarosse Nyamubi,wakati akizungumza na jumuiya ya wazazi wanayozunguka shule ya wasichana ya Chief ihunyo katika kijiji cha butuguri wakiwemo  wanafunzi wa shule hiyo,ambapo amesema ifikapo   aprili 30 mwaka huu watoto wote wawe wameripoti katika shule za sekondari walizopangiwa kabla  ya msako huo mkali kuanza.
Kwa upande wake mkuu hiyo ya sekondari hiyo ya wasichana Bi Mary Masansi,ametumia nafasi hiyo  kumpongeza mbunge wa jimbo la musoma vijijini mh nimrod mkono kwa kujenga shule hiyo na  kukabidhi serikalini hatua ambayo imesaidia kuinua elimu kwa watoto wa kike.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment