Mtu mmoja mwanamume
aliyetambulika kwa jina la MUHIDIN SAID, mkazi wa Temeke Jijini Dar es
Salaam, amenusurika kifo jana usiku
usiku baada ya gari alilokuwa akiendesha kuzima
ghafla na hatimaye kuteketea kwa moto katikati ya Coca Cola na Majembe
Mikocheni jijini.
Akizungumzia chanzo cha moto huo
SAID amesema wakati yupo kwenye gari alishangaa ghafla taa zimezima na hivyo
ikamlazimu kushuka na kuangalia sababu za taa kuzima ndipo muda mfupi gari
ikaanza kuungua.
Amesema huenda sababu ya moto huo
ni hitilafu ya umeme kwenye gari.
Mwanamume huyo aliyenusurika
kifo ana umri wa miaka 35 alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T944
BDE.
Amesema alikuwa na gari ya shemeji
yake ambapo alikuwa akitoka Temeke akielekea Kawe kuirudisha ndipo baada ya
matatizo hayo ilimbidi kupaki pembeni kabla ya kuendelea na safari na ndipo
gari kuteketea kwa moto,kwenye gari hiyo alikuwa peke yake na hakuna mtu
aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa na hakuna kitu alichoweza kuokoa ndani ya
gari hiyo dhidi ya maisha yake vitu vingine vyote viliteketea kwa moto.
0 comments:
Post a Comment