Image
Image

Wananchi wahimizwa kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura masasi Mkoani Mtwara


Wananchi katika Halmashauri ya mji wa Masasi Mkoani Mtwara wamehimizwa kuendelea kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa kutumia mfumo mpya wa uandikishaji kwa njia ya kielektroniki BVR Lililoanza Ijumaa iliyopita wilayani humo.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi, MZENGA TWALIB ambaye ameeleza kuwa Halmashauri hiyo imeamua uandikishaji katika Daftari hilo la kudumu uanze kwenye Kata nne za  Chanikanguo, Jida, Mtandi na Mkuti,ambako kuna vituo 28.

Amesem zoezi hilo katika kata hizo ni la wiki moja kabla ya kuhamia kwenye Kata nyingine  zikiwemo Napupa, Mumbaka , Nyasa na Marika.

Kwa mujibu wa TWALIBU hadi sasa zoezi linaendelea vizuri ingawaje kuna matatizo mbalimbali ambayo wakishirikiana na Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wanayapatia ufumbuzi wake.

Halmashauri ya Mji wa Masasi yenye Kata 14 ni miongoni mwa Halmashauri saba zilizopo Mkoani Mtwara ambapo wanachi takriban Elfu-83 na 798 wanatarajiwa kuandikishwa kwenye zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kukamilika katika Halmashauri hiyo hapo tarehe 27 mwezi ujao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment