Balozi Rajabu Hassan Gamaha
Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Balozi Rajabu Hassan Gamaha kuwa Balozi
wa Tanzania nchini Burundi.
Balozi Gamaha
anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Mwasi
Nzagi ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi
huo Balozi Gamaha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa. Uteuzi huo unaanza mara moja.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
27 Aprili 2015
0 comments:
Post a Comment