Mkurugenzi wa mawasiliano ya
Rais,Ikulu, Salvatory Rweyemamu.
Habari hizo ziliripotiwa na
gazeti la TAIFA IMARA ambazo zilikuwa na kichwa cha habari ZITTO AMCHONGEA
MENGI KWA JK na kudai kunasa mazungumzo kati ya Rais Kikwete na kiongozi wa
chama cha ACT-WAZALENDO, Zitto Kabwe ambaye kwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti
wa PAC, ambaye inadaiwa alimchongea kwake kwamba, ndiye kinara anayesababisha
serikali yake iyumbe kila mara.
Mkurugenzi wa mawasiliano ya
Rais,Ikulu, Salvatory Rweyemamu, amewaeleza wandishi wa habari jijini dar es
salaam kuwa Rais aliposikia habari hizo akiwa nje ya nchi alishtushwa nazo na
kwamba Rais hawezi kushiriki njama za kumdhuru raia na kuongeza kuwa habari
hizo ni za kutengenezwa kwa nia mbaya ya kuharibu uhusiano mzuri uliopo kati ya
Rais na Dk. Mengi.
Akizungumzia suala la Rais
kusaini au kutokusaini miswada mbalimbali iliyopitishwa na bunge ukiwemo wa
takwimu na makosa ya mtandaoni ambazo baadhi ya wadau wa habari na tasisi
mbalimbali zimekuwa zikimsihi Rais asisaini hadi zifanyiwe marekebisho
Rweyemamu amesema Rais atasaini yote kwani ilipitia taratibu zote.
0 comments:
Post a Comment