Wananchi hao wamevamia ofisi hizo
huku wakiimba nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikishinikiza kulipwa madai yao
ambapo wamedai kuwa tangu waondoke kwenye maeneo yao kupisha mradi ni zaidi ya
miaka kumi hawajalipwa licha ya Rais kuwaahidi kuwa hawataachwa bila kulipwa.
Kufuatia hali hiyo naibu waziri
wa wizara hiyo Mh. Anjela Kairuki amelazimika kutoka ofisini na kuzungumza na
wananchi hao ambapo amekutana na wakati mgumu kwani kila alipotaka kuzungumza
nao baadhi yao walionekana kutoridhishwa na majibu yake na kuanza kumzomea, na
baade aliweza kuwatuliza kwa kuwaeleza kuwa ndani ya siku saba watakwenda eneo
husika kuzungumza nao.
Hata hivyo licha ya Mh.Kairuki
kutoa kauli hiyo baadhi ya wananchi wamemweleza kuwa wakati wanamsubiri
wanarudi kwenye maeneo yao huku wakitishia kusimamisha mradi hadi watakapolipwa
fedha zao, ambapo kutokana na hali hiyo polisi walionekana kutanda katika eneo
la wizara ya hiyo huku wengine wakiwa na silaha za moto.
0 comments:
Post a Comment