Wananchi wa kijiji cha Mawengi kata ya
Mawengi katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamemlalamikia mwenyekiti wao wa
kijiji Bwana Renatho Kahako kwa kula fedha za michango zinazochangwa na
wananchi kwa ajili ya maendeleo huku pia wakimtuhumu kutotoa taarifa ya mapato
na matumizi ya kijiji kwa muda mrefu.
Wananchi hao wametoa malalamiko hayo mbele
ya mbunge wa jimbo la Ludewa, Mh. Deo Filikunjombe ambaye naye ameungana na
wananchi kumkana mwenyekiti huyo na kudai hafai kuwa kiongozi.
Siku nne za ziara ya Mh.Deo Filikunjombe kuzungumza na wananchi
pamoja na kutekeleza shughuli zake mbalimbali za maendeleo wilayani Ludewa,
zikamfikisha katika kijiji hiki cha mawengi, hapa bila kuchelea wananchi
wakatua malalamiko dhidi ya viongozi wao akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho
bwana renatho kahako.
Hali hiyo ikaibua hasira kwa Mbubge wa jimbo la Ludewa,Mh.Deo Filikunjombe
ambaye anakiri kumkabidhi bati 100 mwenyekiti wa kijiji cha mawengi kwa ajili
ya ujenzi wa shule ya msingi ya mkumbo tangu mwaka 2012 lakini cha kushangaza
bati hizo hadi leo hazijafika kwa walengwa.
Katika sakata hilo ambalo nyuma yake likabebwa na minong’ono ya
hapa na pale ya wananchi kumkana pia diwani wa kata ya mawengi, Bwana Leodgar Mpambalyoto
kwa tuhuma za kuwa mbali na wananchi, diwani huyo akaruka kihunzi futi 100 na
kujitetea.
Hata hivyo mbunge huyo amewakabidhi vijana wa kikundi cha cycle
star mashine mpya ya kufua UPEPO-COMPRESSOR pamoja na mashine ya kuungia
vyuma-welding ambavyo vitasaidia wananchi na wakulima wa mawengi kutengeneza
vifaa vyao kwa gharama nafuu.
0 comments:
Post a Comment