Serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha
imezionya baadhi ya taasisi zisizo za kiserikali na baadhi ya viongozi ambao
wanadaiwa kuchochea migogoro ndani ya jamii na kuwatetea baadhi ya wageni
wanaoingia nchini kinyume cha sheria wakiwa na makundi ya mifugo hali ambayo
inasababisha uvunjifu wa amani katika eneo la Ngorongoro.
Akiongea na viongozi wa
kimila na baadhi ya viongozi wa serikali wakiwemo madiwani wa halmashauri ya
wilaya ya ngorongoro, mkuu wa wilaya ya Ngorongoro,Hashim Mghandiwa amesema
wilaya ya Ngorongoro imekuwa na sifa mbaya kitaifa na kimataifa kutokana na
changamoto hizo ambazo zinatakiwa kupatiwa ufumbuzi ili eneo hilo liendelee
kuwa na amani na ameonya kuwa kiongozi yeyote atakayesababisha uvunjifu wa
amani atakamatwa na pia ameahidi kuchukua hatua kali dhidi ya taasisi zisizo za
kiserikali ambazo zinakwenda kinyume na katiba zao.
Nao baadhi ya viongozi
wa kimila wa tarafa ya Ngorongoro akiwemo mwenyekiti wa baraza la wafugaji
Metui Ole Shaudo wamekiri kuwepo kwa migogoro ambayo imechangia kuvuruga amani
lakini pia wamewalaumu baadhi ya wawekezaji ambao nao wamekuwa kichocheo cha
migogoro kwa wananchi kutokana na kupanua maeneo na baadhi kuyatumia kinyume na
malengo yaliyomo kwenye mikataba yao.
Katikia mkutano huo
baadhi ya viongozi wa kimilia wameiomba serikali kuwashirikisha kikamilifu
viongozi wa jamii kwani wanajua matatizo mengi na mbinu za kuyatatua kama njia
muhimu ya kuimarisha ulizi na usalama wa wananchi wa wilaya hiyo ya Ngorongoro.
0 comments:
Post a Comment