Rais Jakaya Kikwete amewaongoza watanzania katika kuadhimisha dhimisha miaka 51 wa muungano wa
Tanganyika na Zanzibar uliounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maadhimisho hayo kitaifa
yamefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaamna kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE sambamba
na viongozi wengine wa serikali ya jamhuri ya muunganio na Zanzibar Katika
uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuwasili uwanjani hapo
akiwa kwenye gari la wazi akiwa pamoja
na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali DAVIS MWAMUNYANGE, Rais KIKWETE alipokea heshima
kutoka vikosi vya ulinzi na usalama na alipigiwa mizinga 21 na kisha
kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama.
Wengine waliohudhuria sherehe
hizo za maadhimisho hayo ni pamoja
na Makamu wa Rais Dakta MOHAMMED GHARIB
BILAL, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dakta ALI MOHAMMED SHEINna Waziri Mkuu
MIZENGO PINDA.
Wengine ni Rais mstaafu BENJAMIN
MKAPA, AMANI ABEID KARUME na viongozi
mbalimbali wa vyama vya siasa, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini
na wananchi.
Rais JAKAYA KIKWETE ambaye pia ni
Amirijeshi Mkuu anashiriki maadhimisho hayo kwa mara ya mwisho katika nyadhifa
hizo baada ya muhula wake unatarajiwa kwisha baadaeye mwaka huu baada ya
uchaguzi mkuu unaorajaiwa kufanyika Oktoba.
0 comments:
Post a Comment