Mwenyekikti
wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ),Mh. Freeman Mbowe
amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika oktoba 25
mwaka huu licha ya tume ya taifa ya uchaguzi NEC kukabiliwa na upungufu wa
mashine 8000 za BVR ambazo zimesababisha kuchelewa kuanza kwa zoezi la
kuandikisha wap iga kura katika mikoa mingi nchini.
Akihutubia
maelfu ya wananchi wa mkoa wa kagera katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye uwanja wa mashujaa mjini bukoba, Mh. Mbowe amesema ikitokea uchaguzi
mkuu umehairishwa kwa sababu zozote zile, litakuwa ni jambo la aibu katika
jumuiya ya kimataifa kwa kuwa tangu nchi ipate uhuru mwaka 1961, tanzania
haijawahi kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti
huyo wa chadema taifa Mh. Freeman Mbowe ambaye yupo katika ziara ya mikoa ya
kanda ya ziwa amesema tanzania inapaswa kujifunza yanayotokea hivi sasa nchini
burundi ambako rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunzinza anataka kujiongezea muda wa
kutawala baada ya kumaliza awamu zake mbili za uongozi.
Mhadhiri
mwandamizi wa chuo cha josiah kibira cha chuo kikuu cha tumaini makumira
kilichopo bukoba Dk. Azaveli Lwaitama aliyejitambulisha kama mwanachama mfu wa CCM,
amesema awamu ya pili ya ukombozi wa afrika iliyoanza miaka ya 90 inahitaji
nchi kuwa na vyama vilivyo makini ili wananchi wapate maendeleo.
0 comments:
Post a Comment