Kazi kubwa inayoendelea hivi sasa kuhakikisha mradi huu wa umeme
unawafikia wananchi vijijini ukitokea mjini ludewa ni kuchimba mashimo ya
kusimika nguzo za umeme kazi ambayo inafanywa na wananchi kwa kushirikiana na
mbunge wa jimbo la ludewa,Mh. Deo filikunjombe pamoja na mkandarasi aliyepewa
kazi hiyo.
Akishiriki kazi ya kuchimba mashimo na kusimika nguzo za umeme, Mh.Filikunjombe
ambaye amebeba jukumu la kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wake kwa wakati,
amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono katika kujiletea
maendeleo badala ya kuishia kuwa walalamikaji.
Bwana Godson Mshana ni mmoja wa wananchi wa ngalawale-ludewa
aliyejitolea kufyeka mahindi katika shamba lake bila malipo kuunga mkono mradi
huo wa umeme.
Awali akiongea na wananchi
wa vijiji vya lifua, luilo, ngalawale na ngelenge,Mh.Filikunjombe amewatoa wasiwasi
wananchi kuhusu gharama za kujiunga na huduma ya umeme huo pindi
utakapokamilika na kwamba gharama zake zitakuwa shilingi 27,000 tu.
0 comments:
Post a Comment