Wakizungumza kwa jazba huku wakionyesha moja ya shamba
lililoteshwa mbegu hizo ambazo hazikuota
wakulima hao wamesema kwa sasa hawataki tena fidia ya mbegu bali
wanataka fidia ya gharama za kilimo kwani hii nimara pili kupewa mbegu
sizizoota na kwamba kama serikali haitachukua hatua watachukua wao wenyewe .
Akizungumzia malalamiko hayo wakala huyo Bw. Melikizediki Nnko
amesema alishapokea malalamiko hayo na
kuyafikisha kwenye kampuni husika na ikakubali kulipa fidia na hata yeye anashangaa kuona kuwa hata mbegu walizofidiwa hazioti.
Afisa kilimo wa halmashauri ya meru Bi.Grace Solomon amesema
malalamiko hayo pia yalishafika ofidinai kwake na wakalifikisha kwa
wakaguzi wa mbegu
ambao pia walithibitisha
kuwa zilikuwa hazina viwango na kampuni
husika ikatakiwa kuwafidia wakulima hao mchakato ambao bado unaendelea licha ya kukabiliwa na changamoto
nyingi.
0 comments:
Post a Comment