Akiwasilisha matokeo ya
utafiti huo Bi. Rose Aiko
amesema,lengo la utafiti
huo ulikuwa kuangalia wananchi
wana mtizamo gani kuhusu
vyombo vya habari nchini,ambapo baadhi yao wakionyesha
kutofurahia vyombo vya habari
kuripoti matukio mabaya kama ya
ajali za kutisha.
Baadhi ya watu
walioshiriki katika mkutano huo, akiwemo wahariri
na viongozi wa vyama vya
siasa,wamekuwa na maoni
tofauti kuhusu utafiti
huo,huku wengine wakisema kuwa,vyombo vya habari viongozewe
uhuru ili kuweza
kutoa taarifa kwa undani
zaidi na siyo
kutunga sheria ya kuvikandamiza.
Kwa upande wake
mkurugenzi wa utafiti
katika uchumi na maendeleo
wa Repoa Dkt. Donald
Mmari amesema,tafiti nyingi
wanazozifanya zimeisaidia jamii
kuongeza umakini na
kujenga uwezo wa kuhoji mambo mbalimbali
ya maendeleo.
0 comments:
Post a Comment