Kamanda wa polisi mkoani Singida, Thobias Sedoyeka,
amesema kuwa,tukio hilo lilitokea jana, saa 12 alfajiri, huko katika kijiji cha
mtamaa ‘a’, huku akimtaja marehemu huyo aliyejulikana kwa jina la Tausi Abdalah
Miaka Hamsini na Sita, na kueleza kuwa siku ya tukio, kijana huyo alikwenda
nyumbani kwa marehemu saa kuminambili alfajiri, kisha akamchinja au
kumkata shingoni mama yake, ambaye alipoteza uhai papo hapo.
Akifafanua zaidi juu ya tukio hilo,Sedoyeka amesema kuwa,aprili
16 Mwaka huu, mtuhumiwa alifika kwa mama yake na kubomoa sahemu ya nyumba yake,
kabla ya kumkamata mbwa na hatimaye kumchinja, kisha akatokomea zake
kusikojulikana.
Kamanda Sedoyeka amesema kuwa,kutokana na historia ya mtuhumiwa
kufanya fujo mara kwa mara, ndugu walimkamata na kumpeleka Hospitali ya mkoa wa
Singida, lakini baada ya uchunguzi alirejea nyumbani na kutokana na
marehemu kuwa na hofu, ilibidi akalale kwa majirani na siku
iliyofuata,majira ya alfajiri alirejea nyumbani kwake, kwa ajili ya kumjulia
hali kijana huyo, na hapo ndipo alipokamatwa na kuuawa kwa kuchinjwa.
Kamanda Sedoyeka akielezea zaidi amesema kijana huyo baada
ya kumuuwa mama yake alikwenda kwa mama yake mkubwa kutoa tarifa, kisha tena
akaenda kwa mwenyekiti wa kijiji kumjulisha kuwa, amefanya mauaji ya mama
yake,na kabla ya mauaji hayo siku za nyuma mtuhumiwa alifanya tukio la kuwaua
ng’ombe watatu wa mama yake kwa kuwacharanga na panga, wakati wakiwa
machungani.
Hata hivyo, Sedoyeka amesema kuwa, tayari wanamshikilia kijana
huyo, kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ikiwemo kumpeleka hospitalini, ili kupimwa
akili zake,kutokana na tukio hili, sedoyeka amewataka wananchi wa mkoa wa
singida na taifa kwa ujumla, kuchukua tahadhari, dhidi ya ndugu na jamaa,
wanaoonekana kuwa na matatizo mbalimbali, ikiwemo maradhi ya akili.
0 comments:
Post a Comment