Rais Jakaya Kikwete
ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Morogoro katika mazishi ya
aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kyerwa Luten Kanali mstaafu Benedict Kitenga aliezikwa kijeshi katika
makaburi ya kola mjini morogoro.
Akizungumza na waombolezaji
nyumbani kwa marehemu Kola Hill mkoani Morogoro Rais Kikwete amesema serikali
imepoteza kiongozi muhimu aliekuwa mchapakazi ambapo
amewataka ndugu na wanafamilia kuwa na moyo wa uvumilivu hasa katika wakati huu
mgumu wa kuomboleza kifo cha ndugu yao.
Akitoa salamu kwa niaba
ya mkuu wa majeshi majeshi Device Mwamunyange Meja Jenerali
Nerali Salum Kijuu amesema marehemu alilitumikia jeshi la
wananchi JWTZ kwa uadilifu na uaminifu huku mwenykiti wa wakuu wa
wilaya nchini Jason Msome umoja wa wakuu wa wilaya wamestusha na
kifo hicho ambapo wameeleza maerhemu alifanya kazi zake kwa ushirikiano wa
karibu na wenzake hadi umauti ulipo mkuta.
Kwa upande wake ndugu wa
marehemu wameshukuru serikali kwa jitihada za kumuuguza marehemu na
kuiomba serikali kuendelea kuwa karibu na familia ya marehemu katika masuala
mbalimbali hasa katika wakati huu mgumu wa maombolezo huku askofu mkuu wa jimbo
la morogoro Telesphol Mkude amewataka watanzania kufanya matendo yanayompendeza
mwenyezimungu kwani hapa duniani tutaondoka na uzima wa milele upo mbinguni.
Marehemu benedict
kitenga amefariki april 20 katika hospitali ya taifa ya muhimbili na
kuzikwa pril 23 katika makaburi ya kola mjini morogoro ambapo mazishi yake
yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali akiwemo
waziri mkuu mizengo pinda ,waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa
na serikali za mitaa hawa ghasia na waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi
selina kombani wakumuu wa mikoa na wakuu w awilaya .
0 comments:
Post a Comment