Na.Mwandishi wetu Comoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (Mb)
ahudhuria Kongamano Kubwa la Biashara kati ya Comoro na Tanzania,
litakalofanyika tarehe 23 Aprili, 2015 Visiwani Comoro.
Lengo kuu la kongamano
hilo ni “kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro
kwa kutambua fursa zilizopo kati ya nchi hizi mbili na kurasimisha biashara
ambayo kwa sasa hairatibiwi”.
Kongamano
hilo ambalo litawakutanisha viongozi, maafisa wandamizi wenye dhamana ya
kuendeleza biashara kutoka Tanzania na Comoro pamoja na wadau wa Sekta Binafsi, litafungua rasmi fursa ya kutangaza na
kuuza bidhaa zinazozalishwa Tanzania kwa wafanyabiashara watakaopenda kufanya
hivyo kutokana na nafasi nyingi za biashara na uwekezaji zilizopo katika Visiwa
vya Comoro.
Miongoni
mwa mada ambazo zitazungumzwa katika kongamano hilo ni pamoja na; Mada kadhaa kuhusu fursa za biashara na uwekezaji
nchini Tanzania na Comoro, mazingira ya biashara za uwekezaji nchini Tanzania
na Comoro, fursa zinazopatikana katika nchi hizo na usaidizi wa kiserikali
katika kurahisisha baishara. Aidha, itakuwapo fursa ya mazungumzo ya kina kati
ya wafanyabiasha wa Comoro na Tanzania (business to business discussions).
Aidha,
zipo fursa nyingi za uwekezaji katika uzalishaji na usindikaji wa bidhaa za
kilimo, pamoja uwekezaji katika sekta ya huduma za afya, elimu, mawasiliano na nishati
endapo fursa hizi zitatangazwa na kuwekwa miundombinu ya uhakika ya usafiri
kati ya Tanzania na Comoro bidhaa za Tanzania zitapata soko la uhakika visiwani
Comoro.
Kongamano
hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na wafanyabiashara na wadau mbalimbali kutoka Tanzania, limeandaliwa na Ubalozi wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania nchini Comoro, kwa kushirikiana na kampuni ya
361 degrees ya Dar es Salaam. Kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali, ikiwa ni
pamoja na Mamlaka ya Uendelezaji wa Biashara Tanzania (TANTRADE) ambao
wanahamasisha na kuwakaribisha wafanyabiashara wa Tanzania, Exim Bank, Shirika
la Ndege la Air Tanzania, Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima
ya Comoro (UCCIA); na Mamlaka ya Kuendeleza Vitega uchumi vya Comoro (INM).
0 comments:
Post a Comment