Wafanyakazi hao
wawili wa Bonite Bottlers Moshi , ambayo ni moja ya kampuni za IPP, wakiwa
kwenye gari Toyota Hiace ,lenye namba za usajili T 803 ATR , waliuawa na watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi karibu na Kili FM Radio,barabara mpya ya Soweto mjini Moshi mkoa wa
Kilimanjaro.
Watu hao walikuwa wamepanda
pikipiki mbili mojawapo ikiwa ni aina ya Boxer.
Mauaji hayo ya kinyama
yaliyoondoa roho za wafanyakazi hao waliokuwa wakitegemewa na kampuni na familia
zao yanasikitisha sana na Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu hao
mahali pema peponi.
Wakati uchunguzi wa mauaji hayo unafanywa na Polisi,
mtu ye yote mwenye taarifa zozote
kuhusu uhalifu hu o atoe taarifa kituo
chochote cha Polisi hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment