Zifahamu tabia za kimaskini zinavyotutesa Watanzania wengi katika maeneo tofauti tofauti tunapoishi.
Umaskini unaondoa utu, umaskini ni udhalilishaji, umaskini ni uhayawani.Kwa kutambua ubaya wa umasikini, hata vitabu vya dini vinasisitiza waumini kumwomba Mwenyezi Mungu waondokane nao.
Umaskini uwe wa mali au fikra, bado ni tatizo kwa binadamu. Niwatazamapo Watanzania wenzangu nabaki bumbuazi, umaskini umetuathiri, umetuingia kuanzia katika damu hadi akilini.
Kuna wakati, wengi tunafanya mambo kama vile ni majununi au hayawani wa porini.
Hizi ni tabia zinazotokana na umaskini hasa wa fikra.
Naomba kuzitaja baadhi.
Moja, kukimbilia majanga,Kuna tabia ya ajabu ya Watanzania kukimbilia kwenye matukio ya hatari, badala ya kutafuta namna ya kuyaepuka.
Lori la mafuta likipinduka watu watasukumana kuiba mafuta.
Unahatarisha maisha kwa kuchota ndoo moja ya mafuta.
Mwaka 2000 watu zaidi ya 40 walikufa mkoani Mbeya,likajirudia tena Mbagala, litatokea tena tena na tena, tutakufa kwa kuwa hatujifunzi.
Mbili, kukosa ustaarabu katika matumizi ya vyombo vya usafiri. Nimebahatika kutembea nchi kadhaa ndani na nje ya bara la Afrika, Tanzania ni nchi ya kipekee ambayo hata wakati wa kuteremka katika vyombo vya usafiri, watu wanasukumana sikwambii hali ikoje wakati wa kupanda vyombo hivyo.
Kuna watu wamesusa kuwasaidia wananchi wenzao vituoni, kwa sababu wanawatia hasara kwa kuvunja vifaa vya magari.
Gari la abiria wanne, linavamiwa na umati wa watu 3O, kila mmoja anataka kupanda.
Tatu, ulaji wa ovyo.Tunaoishi uswahilini, tunaona Watanzania wasivyojua vibaya wala vizuri katika kula.
Juu ya mtaro wa maji machafu, vyakula tena visivyofunikwa vinauzwa na watu wananunua tena kwa kugombania.
Tamaa ya kupenda vitoweo watu wanakula mpaka viungo vya ajabu vya wanyama hasa ng’ombe.
Haishangazi kuwa mjini sasa nyama za mbwa, paka zinauzwa na kuchangamkiwa.
Nina shaka huko tuendapo,watu tutafikia hatua ya kukaangiza vinyesi.
0 comments:
Post a Comment