Wamedai kuwa kwa muda mrefu
kumekuwepo na upungufu wa wahudumu katika zahanati hiyo huku miundombinu yake
ikiwa chakavu hali ina yo sababisha wagonjwa kuchelewa kupata huduma za afya , hali
inayohatarisha maisha ya wagonjwa na wajawazito.
Wakazi wa Kata ya Ukenyenge
wanaotegemea kupata huduma za afya katika zahanati hiyo wamesema hali hiyo
inawakatisha tamaa kwani hata wananchi waliojiunga katika mpango wa huduma ya
Afya ya Jamii hawapati huduma kama inavyohitajika .
Katika zahanati hiyo baadhi ya majengo yamechakaa na vyoo
naonekana vimedidimia na kuanguka na choo kimoja kinachotumiwa na wagonjwa
pamoja na wahudumu kikiwa na nyufa na
kipo hatarini kuanguka .
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu
Halmashauri ya Kishapu ,Bwana MOHAMED
MLEWA amekiri kuwepo kwa matatizo
hayo, lakini amewatoa hofu wananchi kwa
kusema serikali imeshaanza kushughulikia kero hiyo .
0 comments:
Post a Comment