Kutokana na hali hiyo,
wasichana zaidi ya Elfu-8 hupoteza haki yao ya kupata Elimu kwa
kupata mimba zisizotarajiwa, na pia kuchangia ongezeko kubwa la watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Marie Stopes ,Bi ELLY REWETA ameyasema hayo Mjini Mpanda Mkoani Katavi,
wakati shirika hilo lilipokuwa likizindua rasmi huduma za uzazi wa mpango
kwenye mkoa huo .
Amesema wanawake 255 kati ya kila
wanawake Laki-Moja h upoteza maisha kila mwaka kwa ajili ya
uzazi, na wengi wakijifungulia majumbani kwa zaidi ya asilimia 60, na kusema
kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuifikisha eli mu hiyo ya afya ya uzazi hadi shuleni ili kuwaokoa vijana wengi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda ,Bwana PAZA MWAMLIMA,
akimwakilisha mkuu wa mkoa huo wa Katavi ,
Dakta IBRAHIM MSENGI katika uzinduzi huo, ametoa wito kwa jamii ya mkoa
huo kutumia kwa dhati huduma za uzazi wa mpango zinazotolewa na Marie Stopes .
0 comments:
Post a Comment