Mkemia mkuu wa serikali, Prof. Manyele ameyasema hayo jijini mbeya
wakati akikabidhi vyeti vya usajili wa muda kwa wasafirishaji,wauzaji na
wasambazaji wa kemikali za aina mbalimali mkoani mbeya.
Baadhi ya wasafirishaji,wauzaj na wasambazaji wa kemikali mkoani
mbeya wamesema hatua ya wao kupewa vyeti hivyo imewafurahisha kwa kuwa sasa
watafanya kazi hiyo wakiwa huru na kwa kufuata sheria na taratibu za nchi.
Katika miaka ya hivi karibuni,kemikali zimekuwa zikitumika vibaya
kwa kuwepo matukio ya watu kumwagiwa tindikali, na kusababishiwa madhara
makubwa, hali ambayo imeilazimu serikali kuchukua hatua za kukabiliana na hali
hiyo.
0 comments:
Post a Comment