Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa
Kenya Bi AMINA MOHAMED baada ya kukutana na waziri mwenzake wa Somalia na
mwakilishi wa shirika la wakimbizi amesema kwenye kamati hiyo kila upande
utateua wawakilishi wanne.
Kenya inataka kufungwa kwa kambi
ya wakimbizi ya Dadaab Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo na ambayo ni kubwa
zaidi barani Afrika na duniani kwa jumla kwa madai ya kutumika kupanga
mashambulio ya kigaidi nchini humo.
Tarehe pili mwezi huu Naibu Rais
Bwana WILLIAM RUTO alitoa siku 90 kufungwa kwa kambi hiyo yenye wakimbizi
wapatao 350,000 wengi wao wakiwa Wasomalia baada ya shambulio la mwezi uliopita
kwenye Chuo Kikuu cha Garissa ambapo watu 150 wengi wao wanafunzi waliuawa.
0 comments:
Post a Comment